TAARIFA KUHUSU ENEO LA UJENZI WA WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA MJINI DODOMA.

0
156
Katibu Mkuu wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia  Maimuna Tarishi, leo amekabidhi eneo la kiwanja kwa Wakala wa Majengo Tanzania ili wakala hao  waandae  mpango wa matumizi ya eneo hilo kwenye makao makuu ya nchi mjini Dodoma.

Katibu Mkuu Tarishi ameelekeza kuwa eneo hilo ni maalumu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi zitakazotumiwa na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  kama vile Mamlaka ya Elimu Tanzania, -TEA, Bodi ya Mikopo -HESLB, na Tume ya Vyuo Vikuu nchini -TCU. 

Katibu Mkuu Tarishi ameiagiza TBA  kuandaa  Michoro ( Design) na Kufanya ujenzi wa majengo ya Ofisi za wizara hiyo ujenzi ambao utafanyika Kwa Awamu.

TBA imesisitizwa kukamilisha ujenzi mapema iwezekanavyo Kwa mujibu wa makubaliano.
Kwa taarifa zaidi bofya link ifuatayo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here