TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTOAJI WA VYETI VYA WAHITIMU WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KATIKA PROGRAMU ZA AFYA, MIFUGO NA UALIMU KWA MWAKA WA MASOMO 2015/2016

0
99

Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria
ya Bunge, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu na mafunzo
ya ufundi nchini. 

NACTE ina
wajibu wa kutunuku vyeti kwa wahitimu wenye sifa stahiki kwa mafunzo ya
programu za Afya, Mifugo na Ualimu yanayozingatia umahiri.

Tarehe 14
Julai 2017 Baraza lilitoa taarifa kwa umma kuwa vyeti vya wahitimu wa
mafunzo ya programu za Afya, Mifugo na Ualimu wenye sifa stahiki kwa
mwaka wa masomo 2015/16 vingeweza kutolewa muda wowote ndani ya Mwezi wa
Julai 2017. Kwa sababu za kiufundi, vyeti hivyo havikutolewa kama
ilivyoahidiwa. Hata hivyo, Baraza linatarajia kuwa vyeti vitakuwa tayari
ifikapo tarehe 12 Agosti 2017.

Kuhusu uthibitisho wa wanafunzi kuhitimu mafunzo ya taaluma husika, wahitimu wanashauriwa kuomba ‘transcripts’ kupitia tovuti ya NACTE www.nacte.go.tz
na transcripts ni uthibitisho halisi wa uhitimu wa mwanafunzi. Baraza
linaendelea na zoezi la utoaji wa transcript kwa wahitimu wote kulingana
na maombi yanavyowasilishwa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 01/08/2017

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here