Description
Kiswahili shule ya sekondari kidato cha pili kimeandikwa kwa mujibu wa muhtasari mpya wa mwaka 2005 wa somo la Kiswahili kwa shule za sekondari Tanzania. Kitabu hiki kimezingatia sana mahitaji ya wanafunzi darasani na ya taifa kwa ujumla.
Katika kitabu hiki, wanafunzi watapata nafasi ya kuzielewa kwa kina mada zote za lugha ya Kiswahili kwa kidato hiki ambazo ni
- Uundaji wa maneno
- Matumizi ya lugha katika miktadha mbalimbali
- Uhakiki wa kazi za fasihi simulizi
- Uhifadhi wa kazi za fasihi andishi
- Utungaji wa kazi ya fasihi simulizi
- Uandishi
- Usimulizi
- Ufahamu
Katika katika kila sura kuna maswali kadhaa ambayo yamekusudiwa kuwasaidia wanafunzi kupima uwezo wao wa kuelewa walivyo jifunza.
Aidha, kwa kuwa wanafunzi wa kidato cha pili wanakabiliwa na mitihani ya taifa, imeonelewa mwishoni mwa kitabu hiki, kuwe na mifano ya maswali ya mitihani ya Kiswahili ambayo yatawasaidia wanafunzi katika kujiandaa kwa mitihani hiyo.
Vitabu vingine katika mfululizo huu ni,
Kiswahili shule za sekondari, kidato cha kwanza
Kiswahili shule za sekondari, kidato cha Tatu
Kiswahili Shule za sekondari Kidato cha Nne
Reviews
There are no reviews yet.