Description
Wanawake wengi sana wana uwezo mkubwa sana ndani yao ila wanashindwa kabisa kufanya mambo makubwa katika maisha yao, matokeo yake wanaishi maisha ya kawaida. Ikitumika mifano mbalimbali ya wanawake wa Kitanzania na mataifa mengine ambao wamefanikiwa kutimiza malengo makubwa kwenye maisha yao, kitabu hiki kitakufundisha.
- Kuzijua nguvu 6 za kipekee ambazo mwanamke anazo na jinsi ya kuzitumia
- Kutambua vikwazo ambavyo vinawakwamisha wanawake wengi na jinsi ya kukabiliana navyo
- Hatua za kutoka katika maumivu ya kihisia ambayo yanaumiza wanawake wengi
- Mbinu za kufanikiwa kibiashara na kifedha kwa mwanamke
- Mambo ya kufanya ili ujitofautishe kwa haraka katika unachokifanya
- Aina za marafiki kwa wanawake na jinsi ya kuchagua rafiki sahihi n.k
Baada ya kusoma kitabu hiki utabadilika na kuwa mwanamke ambaye unatimiza malengo yako na hauta kwamishwa na vikwazo ambavyo vimekuwa vinawakwamisha watu wengi. Utakuwa ni mwanamke ambaye hisia zake zimeponywa na utajua namna ya kuondokana na maumivu yoyote yatakayo jitokeza katika maisha yako.
Reviews
There are no reviews yet.