Home Shop BOOKS Life Matters TIMIZA MALENGO YAKO

TIMIZA MALENGO YAKO

Sh15,000

Mwandishi wa kitabu: Joel Arthur Nanauka

Jina la kitabu: Timiza Malengo yako

Katika kitabu hiki kuna Mbinu walizo zitumia watu maarufu kufanikiwa.

Categories: ,

Description

Mwandishi wa kitabu: Joel Arthur Nanauka.

Jina la kitabu: Timiza Malengo yako

Katika kitabu hiki kuna Mbinu walizo zitumia watu maarufu kufanikiwa.

TIMIZA MALENGO YAKO ni kitabu ambacho kinatoa mbinu ambazo watu wengi wamezitumia na wanaendelea kuzitumia duniani kote ili kufikia malengo waliyo jikiwekea katika maisha yao. Ukweli ni kuwa watu hawashindwi kutimiza malengo yao kwasababu hawana uwezo na shauku ya kufanya hivyo, bali kwasababu wameshindwa kujua wafanye nini ili kutimiza malengo waliyo nayo katika maisha yao.

Kama ulishawahi kuweka malengo na yakashindwa kufanikiwa basi unaweza kuanza ukurasa mpya wa maisha yako na ukaungana na wale ambao kila wakati malengo yao huwa yanafanikiwa.

Katika kitabu hiki utajifunza mambo kadhaa ikiwemo

  • Namna ya kuweka malengo yanayofanikiwa¬†
  • Mambo ya kufanya kila siku ili uharakishe mafanikio yako
  • Mbinu za kutumia ili kuepuka umaskini kwenye maisha yako
  • Kujua kusudi lililofanya uzaliwe
  • Mbinu za kuibadilisha ndoto yako kuwa uhalisia
  • Sabababu zinazowafanya watu wafeli na jinsi ya kuziepuka n.k

Hakuna mtu aliyeumbwa kushindwa katika maiosha yake, hakuna mtu aliyezaliwa ili kuteseka katika maisha. Kila mtu amezaliwa na uwezo wa kipekee ndani yake ambao akijitoa kuutumia basi maisha yake yatabadilika na kuwa ya mafanikio sana. Sina shaka kuwa kitabu hiki kitafungua ukurasa mpya katika maisha yako ya kufanikiwa katika malengo yako yote uliyo nayo.

Kumbuka kuwa kila lengo ulilonalo maishani mwako linaweza kufanikiwa kama utajifunza na kuyatumia yaliyo andikwa humu.

 

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “TIMIZA MALENGO YAKO”

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!